Hakika Allah Ni Aliye juu ya Waliojuu Aliye tukuka...
“Aliye juu ya Waliojuu Aliye tukuka” ... Yuko Na utukufu kamili katika sura zote, utukufu Wa dhati, utukufu Wa uwezo Wake Na sifa zake utukufu Wa kuteza nguvu kWake. {Na Yeye ndiye aliye juu, Na ndiye Mkuu} (Al-baqarah: 255), Amestawi juu ya arshi, Na Kwa sifa zote tukufu, Na ukubWa Na heshima zote Na uzuri alisifika, Na kWake ndio zimekamilika.
“Aliye juu ya Walio juu” ... Ametakasika Na kila sifa ambayo hailingaNi Naye, Na kila upungufu wenye kutokea, imetakasika dhati yake Na sifa zake Na uwezo Wake, Ni Allah aliyetukuka.
Hakika Allah Ni Aliye juu ya Walio juu Aliyetukuka …