Hakika yeye Ni Allah Mwenye kumiliki: {Mfalme, Mtakatifu} (Al-hashri: 23)
“Mfalme Mwenye kumiliki”… Ambaye aNa ufalme, aNasifika kWa sifa ya kumiliki, Nayo Ni sifa ya ukubWa Na utukufu Na nguvu Na kupanga, Ambaye ndiye mfanyaji Wa vitu kWa hakika bila mipaka, katika kuumba Na kuamrisha Na kulipa, Na ulimwengu wote Wa chiNi Na Wajuu Ni Wake yeye, wote Ni Waja Wake Na wenye kumilikiWa Naye, Na wenye kumuhitaji yeye.“Mfalme”… Mwenye ukubWa Na utaWala aNapanga mambo ya Waja Wake Na aNafanya atakavyo, kWaNi Wao Ni Waja Wake Na WaNamuhitaji yeye, Naye Ni Mfalme Wao Na Mwenye KuWamiliki.
ANao utaWala Wa hakika, kWasababu hakuNa Mfalme Wala Raisi isipokuWa Naye Ni mmilikiWa Na yeye, hakuNa heri yoyote duNiaNi Wala akhera isipokuWa iNatoka kWake Na Ni fadhila zake. {Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguNi Na duNiaNi.} (Al-baqarah: 255)
“Mfalme” … ANatoa bila hesabu, Na aNaWapatia Kwa kumWaga Waja Wake, Wala hakipungui chochote katika milki yake, Wala halimshughulishi jambo lolote akaacha lengine. Katika hadiith qudsi sahihi amesema Allah: &" Lau WamWanzo wenu Na Wa mwisho wenu, Na WaNadamu wote Na majiNi wote Watasimama katika uWanja mmoja Na wote WaNiombe Na Nimpe kila aliyeomba alichokiomba haipunguzi lolote katika haziNa yangu, bali Ni mfano Wa kuingiza sindano kwenye bahari Na itoke Na toNi &" (ImepokeWa Na Muslim)
“Mfalme” … Humpa ufalme Wake amtakaye. Amesema Allah Mtukufu: {Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, Na humwondolea ufalme umtakaye, Na humtukuza umtakaye, Na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikonoNi mWako. Hakika Wewe Ni Muweza WA kila kitu} [aali’imran: 26]
“Mfalme” … Mwenye kuWamiliki Waja Wake aNayeendesha mambo Yao ya duNia Na akhera; basi yeye yapasWa apendwe Na ukusudiwe, Na Watu Waongeze tamaa ya kuyaomba yaliyo kWake, Kwa kuomba Na kutaka Na kulalamikia Na kumuita yeye Allah pekee.
Hakika yeye Ni Allah Mwenye hekima Mwenye kuhukumu …