{Na Mwenyezi Mungu anakutahadharisheni na adhabu zake} [aali imran :30]
Khofu ya Allah ni miongoni mwa ibada za moyo zilizo kubwa, amesema Allah Mtukufu: {Hakika huyo ni Shet'ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.} [Aali Imran : 175]
Katika aya hii kunaulazima wa kumuogopa Allah pekee. na kukokoteza kuwa kumuogopa Allah ni miongoni mwa misingi ya imani, na kadri imani ya mja itakuwa kubwa ndiyo khofu yake kwa Allah nayo inakuwa kubwa.
Kutoka kwa mama Aisha [r.a] amesema:«Nilimuuliza Mtume[s.a.w] kuhusu ayah hii» {Na hao ambao wanatoa [zaka na sadaka katika mali] waliyopewa, na hali nyoyo zao zinaogopa}«JE niwale wanao kunywa pombe na kuiba ? akasema : ” la! Ewe Binti wa As-Swidik, ni wale ambao wanafunga na wanaswali na wanatoa zaka nao wanaogopa zisijekutotakabaliwa aamali zao» (Imepokewa na Atirmidhi)
Amesema Allah Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu anakutahadharisheni na adhabu zake} [Aali Imran :28]
Akasema Allah Mtukufu: {Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume.} [Az-zumar : 67]
Khofu ya Allah inalazimu elimu ya kumtambua Allah, na elimu ya kumtambua Allah inalazimu kumkhofu , na kumkhofu Allah inalazimu kumtii.}
Hivi ndivyo inalazimu khofu ya Allah, amesema Mtume [s.a.w] «Kithirisheni sana kukumbuka kivunja ladha zote [mauti] kwasababu hakuna anayeyakumbuka awe katika maisha ya dhiki isipokuwa Allah atayakunjua, au awe katika maisha ya wasaa isipokuwa Allah atayadhiki» (Imepokewa na Atabarani)
Na kutoka kwa Baraa [r.a] amesema: «Tulikuwa na Mtume [s.a.w] katika Jeneza, akakaa pembezoni mwa kaburi, kisha akalia paka mchanga ukalowana machozi, kisha akasema: “Enyi ndugu zangu mfano wa safari hii mjiandae nayo»
(Imepokewa na Ibn Majah)
Na amesema Allah Mtukufu: {Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi, na iogopeni siku ambayo mzazi hatamfaa mwana, wala mwana hatamfaa mzazi kwa lolote. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala asikudanganyeni na Mwenyezi Mungu mdanganyifu.} [Luqman :33]
[An nisaa :56]
Aakasema tena : {Na waonye siku ya majuto} [Maryam :39]
a-Kuogopa adhabu yake
Adhabu ambayo aliwaahidi wanaomshirikisha na kitu chochote na wale wanaomuasi na kujieka mbali na twaa yake.
b-Kumuogopa Allah:
Nayo ni khofu ya wanavuoni wanaomtambua Allah vizuri. {Na Mwenyezi Mungu anakutahadharisheni na adhabu yake,} [Aali Imran : 28]
Na kila mtu anapozidi kumtambua Allah huzidi kumcha, amesema Allah Mtukufu: {Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu [wanavyuoni]} [Fatir: 28]
Kwasababu walipo mtambua Allah kwa ukamilifu, kwa kuyajua majina yake na sifa zake, elimu hii ikazalisha khofu ya Allah, na athari zake zikaingia moyoni kisha zikadhihirika kwa vitendo.
Khofu itakapotulia kifuani mwa a.
MIONGONI MWA MATUNDA YA KHOFU YA ALLAH:
a-duniani:
Akasema tena: {Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni * Watu
ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka.} [An nur: 36-37]
Nyoyo zitadahadari na kuwa na wasiwasi na kuogopa, na khofu ya kuogopa siku hio ndio imewapelekea kutenda vitendo vyema, wakitaka kuepukana na shida hizo wakitahadhari maangamivu ya siku hio wakiechelea kupewa vitabu vyao kwa mikono yao yakushoto.
Khofu itakapo tulia kifuani mwa mtu huchoma matamanio yake na kufukuza kupenda dunia.
Mwenye kumuogopa Allah khofu yake itamwelekeza katika kila la kheri.
b-Akhera :
Dhahiri ya maneno haya yanatoka ulimini mwake kwa ajili ya kumuogopesha mwanamke huyo kutokamana na kitendo chake hicho cha kumtaka mtu huyo kwa uchafu, na kuikumbusha nafsi yake na kubaki katika msimamo wake huo bila kurudi nyuma baada ya maamuzi ya mwanzo. « na mtu aliyemtaja Allah akiwa pekee, mpaka machozi yakambubujika»
(Imepokewa na Albukhari)
Kuogopa Allah kunasababisha kutokwa na machozi, na macho yatakayo tokwa na machozi kwa ajili ya Allah basi hayataguswa na moto siku ya kiyama
Allah akampatia udhuri kwa ujinga wake, na khofu yake kwa Allah ikawa ni sababu ya kusamehewa, [kwasababu kama angelikuwa na elimu asingepata msamaha] kwasababu dhahirri ya vitendo hivi nikuepa kufufuliwa, na tunajua kuwa yoyote atakaye pinga kufufuliwa ni kafiri.
wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.} [Al-ahzab : 35]
Yote haya ni maneno matakatifu yanayokusanya sifa za waumini.
Amesema Allah Mtukufu: { Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku}
[As-sajdah: 16]
Akasema tena: {Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake Mlezi...Sema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili.} [Az-zumar: 9]
Na akasema {Na ambao wanaiogopa adhabu [itokayo] kwa Mola. Hakika adhabu ya Mola wao si ya kusalimika nayo mtu [mbaya]} Al ma ‘arij: 27-28
Na Allah akawasifu waja wake walioko karibu zaidi, nao ni manabii, kwa khofu waliokuwanayo: {Bila shaka wao walikuwa wepesi wakufanya wema, na wakituomba kwa shauku na khofu.} [AL-ambiyaa :90]
Pia malaika wenyewe wanamuogopa Allah Mola wao, amesema Allah Mtukufu: {wanamuogopa Mola wao aliye juu yao, na wanatenda wanayoamrishwa.} [An nahl : 50]
Hakika wanaomtambua Allah ndivyo wanavyo mfanyia aamali na ndivyo wanavyo mtarajia , isipokuwa wanamuogopa Allah na wananyenyekea kwake sana katika sampuli zote za kunyenyekea. Kwa mfano:
Kulia kwake Mtume [s.a.w] akiwa anasali paka inasikika kutoka kifuani mwake sauti ya kwikwi, kama maji yachemkayo kwenye chungu. [Amepokea Ahmad, na Abuudauwd,na Annasaii]
Abubakar anashika ulimi wake huku akisema : «Huu ndio ulioniingiza katika maangamivu’ Huku akisema :‘ “laiti ningelikuwa mti wenyekuliwa na kuisha.» Umar Ibn khatab [r.a] anasema: «Laiti sikuwa chochote chenye kutajwa, laiti mamayangu hakunizaa»Anasema tena: «Kama ngamia aliyepotea atakufa huko kwenye mto wa Furat namimi ndio kiongozi wawaislamu ningeogopa kuulizwa na Allah siku ya kiyama»Na anasema: «Kama kutanadiwa mbinguni, kusemwe ‘enyi watu nyote mtaingia peponi ila mtu mmoja tu’ naogopa huyo mmoja anaweza kuwa mimi»
Uthman Ibn A’fan[r.a] amesema: «Ningependa nikifa nisifufuliwe»
Huyu ni Yule alikuwa akipitisha usiku mzima kwa kumsabihi Allah na kusali na kusoma Quran.
Mama wa waislamu Aisha [r.a] anasoma kauli yake Allah Mtukufu: {Basi Mwenyezi Mungu ametufanyia ihsani, [ametutia peponi] na ametuokoa na adhabu ya pepo moto} [At-tur :27]
Akiwa katika sala yake kisha akalia sana. {Ikiwa utawaadhibu, basi bila shaka hao ni waja wako; na ukiwasamehe basi kwa hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima; [Al-maidah :118]
Khofu kwa Allah imeegemezwa na kumtambua Allah, amesema Mtume[s.a.w] « wallahi mimi nimcha Mungu zaidi kuwaliko na kumuogopa zaidi yenu» (Imepokewa na Muslim)
Kadri ya kumtambua Allah na kujua majina yake na sifa zake na ukamilifu wake na utukufu wake ndio kadri itakuwa khofu kwake na kumuogopa.
{Kwa hakika wanaomuogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu [wanavyuoni]. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu ,Msamehevu}[fatir : 28]
Mwenye kumuogopa Allah hakuna atakaye mdhuru, na mwenye kumuogopa asiye kuwa Allah hakuna atakaye mnufaisha.
Kutoka kwa Al-fudheil Ibn Iyaadh.