Fadhila za (laailaha ila Allah)

Fadhila za (laailaha ila Allah)

Fadhila za (laailaha ILA Allah)

Amesema Mtume Wa Allah (S.A.W) “ Umejengwa Uislamu Kwa Mambo Matano: Kushudia Kuwa Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Isipokuwa Allah, Na Muhamad Ni Mtume Wake , Na Kusimamisha Swala Na Kutoa Zaka Na Kuhiji Na Kufunga Mwezi Wa Ramadhani” (Amepokea Bukhari)

Akasema Tena Mtume (S.A.W) &" Neno Bora Nililolisema Mimi Na Manabii Wote Walionitangulia Ni: (Laailaha Ila Allah Wahadahu Laasharika Lahu Lahu-L Mulku Walahu-L Hamdu Wahuwa Aalakuli Shain Qadiir)Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Ila Allah Peke Yake Hana Mshirika, Ufalme Ni Wake Na Sifa Njema Zake Naye Ni Muweza Wa Kila Kitu. &" (Imepokewa Na Atirmidhiyu)

‘Laailaha Ila Allah’, Kwa Ajili Yake Alipamba Allah Pepo Na Kuchochea Moto Kisha Akaweka Soko La Mambo Mema Na Maovu.

Akasema Mtume (S.A.W) &" Hakika Mtume Nuuh (A.S) Alipojiwa Na Umauti Akamwambia Mwanawe: Nina Kuamrisha Kwa ‘Laailaha Ila Allah’ Kwasababu Kama Itachukuliwa Laailaha Ilaha Ila Allah, Nakuwekwa Kwenye Mizani Na Mbingu Saba Na Ardhi Saba Sehemu Nyingine Ya Miizani, Basi Laailaha Ila Allah Itakuwa Nzito Na Kuangusha Sehemu Ya Pili Ya Mizani, Na Kama Ingelikuwa Mbingu Saba Na Ardhi Saba Ni Kama Pete Isiyojulikana Lailaha Ila Allah Itazishinda Nguvu.&" (Imepokewa Na Bukhari Katika Kitabu Chake Aladabu L- Mufrad)

MASHARTI YA ‘LAAILAHA ILA ALLAH’

1-Elimu Kwa Maana Yake : Nayo Ni Kutambua Mwenye Kuitamka Kalma Hii Ayajue Maana Yake Na Madhumuni Yake Na Vilivyo Ambatana Nayo Miongoni Mwavyo Kukanusha Uungu Wa Asiye Kuwa Allah Nakuuthibitisha Kwake Allah, Amesema Allah Mtukufu: { Jua Ya Kwamba Hakuna Aabudiwaye Kwa Haki Ila Mwenyezi Mungu } (Muhamad : 19)

2-Al-Yaqin : Maana Yake Nikwamba Isipatikane Shaka Yoyote Kwa Mwenye Kutamka Kalima Hii Juu Ya Kalima Yenyewe Au Juu Ya Vinavyo Ambatana Navyo.Kwa Kauli Yake Allah Aliyetukuka { Wenye Kuamini Kweli Kweli Ni Wale Waliomuamini Mwenyezi Mungu Na Mtume Wake;Kisha Wakawa Si Wenye Shaka,Na Wakaipigania Dini Ya Mwenyezi Mungu Kwa Mali Na Nafasi Zao Hao Ndio Wenye Kuamini Kweli. } (Al-Hujurat: 15)

Na Akasema Mtume (S.A.W) ‘ Nashuhudia Kuwa Hakuna Aabudiwae Kwa Haki Ila Allah Na Mimi Ni Mtume Wake Hakuna Atakaye Kutana Na Allah Na Kalima Hii Asiwe Na Shaka Juu Yake Isipokuwa Allah Atamuingiza Peponi.’ (Imepokewa Na Muslim)

3-Kukubali Yaliyo Ambatana Na Hii Kalima Kwa Moyo Na Ulimi: Na Maana Ya Kukubali Hapa Ni Kinyume Cha Kupinga Na Kujivuna Amesema Allah Mtukufu: {Hivyo Ndivyo Tutakavyowafanya Maasi. Wao Walipokuwa Wakiambiwa, Hakuna Aabudiwaye Kwa Haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu,”Walikuwa Wakikataa. } (As-Saaffat: 34-35)

4-Kufuata Yaliyoelekezwa Na Kalima Ya Tawheed : Kwa Maana Mja Awe Anatekeleza Aliyo Amrishwa Na Allah Na Kuachana Na Yote Aliyokatazwa, Amesema Allah Mtukufu : { Na Ajisalimishaye Uso Wake Kwa Mwenyezi Mungu, Na Hali Ya Kuwa Anawafanyia Mema (Viumbe Wenziwe), Bila Shaka Amekwishakamata Fundo Lililo Madhubuti;Na Mwisho Wa Mambo Yote Ni Kwa Mwenyezi Mungu } (Luqman :22)

Hakika Utumwa Wa Kweli Ni Utumwa Wa Moyo, Basi Mwenye Kuumiliki Ndiye Atakuwa Bwana Wa Moyo Huo Nao Utakuwa Mtumwa Kwake.

5-Ukweli: Maana Yake Ni Aitamke Mwenye Kutamka Kalima Kwa Ukweli Kabisa Ndani Ya Moyo Wake, Moyo Wake Ayasemayo Yawafiki Yaliyomo Moyoni Mwake. Amesema Allah Mtukufu: {Na Katika Watu, Wako (Wanafiki) Wasemao: “Tumemuamini Mwenyezi Mungu Na Siku Ya Mwisho”; Na Hali Ya Kuwa Wao Si Wenye Kuamini. Wanatafuta Kumdanganya Mwenyezi Mungu Na Wale Walio Amini, Lakini Hawadanganyi ILA Nafsi Zao; Nao Hawatambui} (Al Baqarah: 8-9)

6-Ikhlaas ( Kumtakasia Allah Ibada) : Nayo Ni Kutaka Radhi Za Allah Katika Kalima Ya Tawhiid, Amesema Allah Mtukufu: { Wala Hawakuamrishwa Ila Kumwabudu Mwenyezi Mungu Kwa Kumtakasia Dini, Waache Dini Za Upotevu, Na Wasimamishe Sala Na Kutoa Zaka- Hiyo Ndiyo Dini Iliyo Sawa. } (A-L Bayyinah: 5)

7-Kuipenda Kalima Hii Ya Tawhiid Na Kuwapenda Watu Wake Wenye Kuifanyia Kazi Na Wenye Kushikamana Nayo, Kwa Sharti Zake, Na Kumbughudhi Kila Mwenye Kuikanusha . Amesema Allah Mtukufu: {Na Katika Watu Wapo Wanao Chukua Waungu Wasio Kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda Kama Kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini Walio Amini Wanampenda Mwenyezi Mungu Zaidi Sana. } {Al-Baqarah: 165}

Hii Ndio Maana Ya (Laailaha ILA Allah) Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki ILA Allah, Na Hizo Ndizo Sharti Zake Ambazo Kwazo Zitakuwa Ni Sababu Ya Kufuzu Mbele Ya Allah. Aliambiwa Hassan Albasriy: Hakika Watu Wanasema : Mtu Akisema Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Ila Allah, Ataingia Peponi , Akasema Mwenye Kusema Hakuna Apaswaye Kuabudiwa Kwa Haki Ila Allah Na Akatekeleza Haki Zake Na Faradhi Zake Ataingia Peponi”

Kila Moyo Ukiongezeka Mapenzi Yakumpenda Allah Huzidi Kumuabudu Na Kuwa Mja Wake Halisi Na Kuwa Huru Na Miungu Wengine Wote.

Kwa Hiyo Kalima Hii Ya Tawhiid Haimfaidishi Mwenye Kuisema Isipokuwa Aifanyie Kazi Kwa Kuleta Sharti Zake, Lakini Mwenye Kuitamka Bila Kuifanyia Kazi Basi Haimnufaishi Na Lolote Mpaka Atakapo Leta Vitendo Viambatane Na Maneno Yake.

VIVUNJA “LAAILAHA ILLA ALLAH”

1. Ushirikina, na unao kusudiwa hapa ni:

Ushirikina ule mkubwa ambao unamtoa mtu katika uislamu, ushirikina ambao Allah hamsamehi mtu atakaye kufa akiwa nao, nao ni kumfanyia Allah kuwa na mshirika katika mambo ambayo ni haki yake

Allah pekee kama ibada na uungu,na majina yake matakatifu . asema Allah Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi [dhambi ya] kushirikishwa na kitu , lakini yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, basi bila shaka yeye amekwishapotea upotofu ulio mbali.} [An nisaa : 116]

Haifai kwa mtu yoyote kumuomba Allah ila kwa majina yake matakatifu, tena kwa maombi ambayo aliyoyaruhusu mwenyewe na kuamrisha ni yale yanayofahamika katika aya hii :

{ Na mwenyezi mungu yuko na majina mazuri basi muombeni kwayo na muache waliokanusha majina yake atawalipa kwa yale waliyokuwa wakiyafanya} [Ala’araaf: 180]

Imamu Abuhanifa

Asema Allah Mtukufu: {Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri. * Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru.}[Az zumar 65-66]/

2. mwenye kujaalia beina yake na Allah wasila akiwaomba kinyume na mwenyezi mungu na akitaka kwao kuokolewa na kuwategemea, basi ameivunja tayari LAAILAHA ILA ALLAH.

3. ambaye hatawakufurisha washirikina au akawa na shaka na ukafiri wao au akayafanya madhehebu yao kuwa sawa basi amekufuru, kwa sababu kwa hayo atakuwa anashaka na yale amabayo yeye yuko nayo yaani uislamu, ambao mwenyezi mungu hakubali dini yoyote ispokuwa hiyo, basi mwenye kuwa na shaka na anayeabudu asiyekuwa Allah au kumfanyia asiye kuwa Allah kitu chochote ambacho anastahiki Allah, au akawa na shaka na ukafiri wa mayahudi na wakristo na washirikina au akawa na shaka kuwa wao ni wa motoni au akasahihisha chochote katika madhehebu ya washirikina na aamali zao ambazo zimekuja dalili zakumkufurisha mwenye kutekeleza vitendo hivyo.

4. mwenye kuitakidi kuwa uongofu wa mtu mwengine umekamilika kuliko uongofu wa Mtume [s.a.w] na kwamba hukumu yake ni bora kuliko hukumu ya Mtume [s.a.w] atakuwa amekufuru, kama mtu anaye fadhilisha hukumu za kanuni au za kitamaduni kuliko hukumu za kisheria ya kiislamu, ama kuitakidi kuwa yafaa kuhukumiwa na kanuni hizo, ama kuziona kuwa ziko sawa na sharia ya kiislamu, huu utakuwa ni ukafiri wa kumkufuru Allah mkubwa . kwa maneno yake Allah Aliyetukuka.: {Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri} [Al-maidah 44]

Na kauli yake Allah: { La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.} [An nisaa : 65]

5. mwenye kuchukia chochote alicho kuja nacho mtume [s.a.w] hata kama ataifanyia kazi basi atakuwa amekufuru, kama mtu atachukia sala hata akisali bado atakuwa kafiri, kwasababu hakupenda aliyo amrisha Allah,kama tujuavyo kuwa miongoni mwa sharti za LAILAHA ILA ALLAH ni kupenda kila kilichokuja kutoka kwa Allah Mtukufu, kwahiyo mwenye kuchukia alichokuja nacho Mtume [s.a.w] ataKuwa haja hakikisha SHAHADATU ANA MUHAMADAN RASUULU ALLAH kwasababu miongoni mwa matakwa yake ni kujisalimisha na kukubali yote aliyokuja nayo Mtume [s.a.w] na kufunguka moyo kwayo.

6. mwenye kufanya mzaha na kitu chochote ambacho kina uhusiano na dini ya Allah au thawabu ama madhambi anakufuru, kwasababu hakuheshimu dini hii ya kiislamu, ambayo alitakiwa kuiheshimu na kumheshimu aliyekuja nayo, kwasababu Allah alihukumu watu walikuwa ni waislamu kuwa wamekufuru walipo fanya mzaha na Mtume [s.a.w] na masahaba wake.walipowaambia “hatujawahi kuona mfano wa wasomi wetu kazi yao ni kula na kudanganya tu na waoga wakifika vitani,

Allah akateremsha kwao: {Na kama ukiwauliza [kwa nini wanaifanyia mzaha dini] wanasema:sisi tulikuwa tukizungumza zungumza na kucheza tu.’”sema: “ mlikuwa mkimfanyia mzaha mwenyezi mungu na aya zake na mtume wake. Msitoe udhuru[wa uongo]umekwisha kudhihirika ukafiri wenu baada ya kule kuamini kwenu.} [At-tawba: 65-66]

Allah alihukumu kuwa wamekufuru ijapokuwa walikuwa kabla ya hapo waislamu, dalili hiyo ni maneno yake Allah aliposema: {Umekwisha kudhihirika ukafiri wenu baada ya kule kuamini kwenu. [At-tawba 66]

Akathibitisha imani yao ya kwanza kabla hawaja sema walio yasema , na akawakufurisha ijapokuwa walisema hivyo kwa njia ya mzaha na mchezo wakikusudia kuvunja ukumya ili watu wafurahi walipokuwa safarini ,

7. uchawi

Navyo ni vifundo na vijikaratasi na vijikambaa vinavyoleta madhara kwa nyoyo za watu na mili yao, wengine waweza kupelekea vifo au kufarikiana kwa wanandoa , nao[uchawi] pia ni ukafiri. Asema Allah Mtukufu: {Na kwa yakini wanajua kwamba aliye khiyari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera.}[Al-baqarah 102]

Fungu au sehemu kisha akasema : {Wala [malaika hao] hawakumfundisha yoyote mpaka wamwambie : hakika sisi ni mtihani basi usikufuru.} [Al-baqarah 102]

Alisema Mtume [s.a.w] «Jiepusheni na madhambi saba yenye kuangamiza, wakasema: ‘ewe Mtume wa Allah ni yapi hayo? Akasema:’ ni kumshirikisha Allah na kufanya uchawi na kuuwa nafsi alizoharimisha Allah kuuliwa ispokuwa kwa haki zake,na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia vitani na kuwasingizia wanawake wakiislamu uchafu ilhaliwenyewe ni wasafi»(Imepokewa na Bukhari)

Akasema tena Mtume [s.a.w] «Mwenye kufunga vifundo kisha akavipulizia basi ameshafanya uchawi, na mwenye kufanya uchawi amemshirikisha Allah na mwenye kujiegemeza na kitu basi atawakilishwa nacho».(Imepokewa na An nasai)

Na miongoni mwa uchawi ni kutizama nyota na falaki na kupiga bao kwa kuangalia matokeo, kama alivyopokea Abuu dawud kutoka kwa Ibn Abas kwamba Mtume [s.a.w] alsema :«Mwenye kuchukuwa elimu ya nyota na falaki basi amechukua elimu ya uchawi na kila akiongeza ndio anazidi kuwa mchawi» (Imepokewa na Albaihaqi)Na amesema Allah Mtukufu: {Wala mchawi hafaulu popote afikapo}[Taha 69]

Elimu iliyo na manufaa ni ile inayomfanya alienayo kumpwekesha Allah, na yanayofungamana nayo katika mambo yenye manufaa kwa watu na kuwafanyia wema. Na elimu inayo dhuru ni ile inayo mpelekea mtu katika ushirikina na kudhuru wenzake wanadamu na kuwakosea.

8. kujifananisha na washirikina na kuwasaidia dhidi ya waislamu; na huku ndiko kuwapenda makafiri alikokutaja Allah katika kauli yake aliposema: {Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki huo nao, basi huyo atakuwa pamoja nao.}[Al-maida 51]

Na ‘atawali’ si kama ‘ muwalat’

kwasababu muwaalat ni kupenda na kuegemea na kusuhubiana, na kufanya hivi bila shaka ni miongoni mwa madhambi makubwa ambayo hayajafika kukufuru, ama atawali ni kumnusuru kafiri na kumsaidia dhidi ya muislamu na kupanga vitimbi dhidi ya muislamu, kama ilivyo kuwa hali ya wanafiki, kwani kuwasaidia washirikina katika mambo ya kidunia mtu atakuwa hatarini.

9. mwenye kudhani kwamba mtu anaweza kutoka katika sharia ya Muhamad[s.a.w] anakufuru kwasababu sharia ya kiislamu aliyokuja nayo Muhamad [s.a.w] ikojuu ya kila sharia na imefuta sharia zote, kwahiyo Allah hakubali isipokuwa sharia ya kiislamu, amesema Allah mwenye nguvu na utukufu: {Bila shaka dini ya haki mbele ya Mwenyezi Mungu ni uislamu }[Aali imran : 19]

Akasema tena: {Na atakaye dini isiyokuwa ya kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye khasara kubwa kabisa} [Aali – imran 85]

Akasema tenaa Allah: {Sema :”ikiwa nyinyi mnampenda mwenyezimungu, basi nifuateni; [hapo] Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu. Na mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira na Mwenye kurehemu. Sema “mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake . Na kama mkikengeuka ,[Mwenyezi Mungu atakutieni adabu] kwani Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.} [AALI- IMRAN 31-32]

Na akasema mtume [s.a.w]«Naapa na Yule ambaye nafsi ya Muhamad iko mikononi mwake , hakuna myahudi wala mkristo atakaye sikia wito wangu huu kisha afe bila kuamini yale niliokuja nayo isipokuwa anakuwa mtu wa motoni»(Imepokewa na muslim)

Mfano wa mambo haya ni kama vile wanavyo dai wale wasio na

Moyo kama hautakuwa safi kwa kuacha ibada ya kila kitu na kuelekea Allah na kuacha kila kitu basi itakuwa ni mushrik

elimu kwamba kuna mawalii ambao wametoka katika kumfuata Mtume [s.a.w] na jambo hili ni ukafiri mkubwa na kutoka katika uislamu.

10. Mwenye kuipa nyongo dini ya Allah yote bila kuifuata atakufuru, na mwenye kuipa nyongo na kukataa kuifata kabisa vingine na kutosheka na vitu au dini ya kikafiri na anapoitwa kwa uislamu na kukumbushwa kufuata mafundisho ya kiislamu anakataa au ajue kisha aipenyongo na aache kuifuata pia amekufuru,

Mambo haya ambayo yana mtoa mtu katika uislamu hakuna tofauti mtu akiwa anafanya mzaha ama yuko kikweli kweli , au muoga watakapo ingia katika mambo haya baada ya kujua kisha wakafanya maksudi , isipokuwa ataye lazimishwa kulazimishwa kwa kutishia maisha yake anajibu kwa ulimi wke tu kama alivyo sema Allah Mtukufu:

{Isipokuwa yule aliye lazimisha na kushindwa nguvu [hana makosa]lakini mwenye kutenda madhambi huku moyo wake unafuraha ndiye atakaye adhibiwa} [An-nahli : 106]

Basi mwenye kulazimishwa kufanya kitendo cha ukafiri kisha akafanya kwa ridhaa yake basi atakuwa amekufuru,kwasababu atakuwa amefanya kwa moyo mkunjufu , ama atakaye kifanya kwa kuzuia khatari ya kuuliwa ilhali imani yake haina dosari basi atakuwa amesalimika na hana atia yoyote, amesema Allah mtukufu: {Ila kwa ajili ya kujilinda na shari zao.} [Aali imran : 28]

Elimu ni mti unatoa kila tabia nzuri, na matendo mazuri , na sifa zakupendeza, na ujinga ni mti unaotoa kila aina ya tabia mbaya na sifa mbovu.

Marejeo

Ni nini maana ya kalima ya tawheed “ LAAILAHA ILA ALLAH “ na nizipi nguzo zake? Na nizipi shuruti zake?

Taja baadhi ya mambo yanayo vunja “ LAILAHA ILA ALLAH” huenda yakawa katika maisha yako au katika jamii yako.

 



Tags: