KUTARAJIA

KUTARAJIA

Amesema Mtume [s.a.w] “fanyieni watu wepesi msiwafanyie ugumu , wapeni watu bishara njema wala msiwakimbize,” imepokewa na Albukhari

Maelezo yake

Kutarajia ni:

Kuhisi kuwepo kwa Allah na fadhila zake na rehema zake, na kuwa na utulivu katika kuona ukarimu wake na neema zake, na kuwa na uhakika kwa hilo, nayo ni muelekezo weye kuelekeza nyoyo kwa Allah na kuzielekeza peponi. Amesema Allah Mtukufu: { Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.}
[An nisaa : 110]

Aina zake

Kutarajia kuko aina tatu, aina mbili zafaa na aina moja haifai bali ni mchezo:

  1. kutarajia thawabu za Allah kwa kutenda vitendo vizuri na kumtii Allah kwa muongozo unaotoka kwake.
  2. kutarajia msamaha wa Allah kwa mwenye kutenda makosa kisha akatubia akitarajia kufutiwa dhambi zake na kusamehewa na kusitiriwa.
  3. kutarajia rehema za Allah kwa mwenye kuendelea na maasi na madhambi kisha anatarajia msamaha na rehema za Allah akiwa katika hali hii tena bila ya aamali zozote, huu ni mchezo na matamanio potevu haiwezi kuwa kutarajia huku kunakubalika kabisa, kutaraji kwa waumini ni kutaraji kuliko shikamana na matendo, amesema Allah Mtukufu: {Hakika wale walioamini na wale waliohajiri[wakahama kuja madina] na wakapigania njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanaotumai rehema za mwenyezi mungu .na mwenyezi mungu ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu.} [Al baqarah : 218]

Daraja zake

Kutarajia [kutumai]kuna daraja inaongezeka na kupanda kulingana na watu wenyewe. Nahizi daraja ni:

  1. kutarajia kunamsukuma mtu kujitahidi katika ibada, na kunaleta utamu wakati wa kutekeleza ibada Fulani hata kama ibada itakuwa nzito kiwango gani kiwango kumueka mtu mbali na maasi na maovu.
  2. kutaraji kwa wenye ijtihadi kuwacha vitu walivyo vizoewa na nafsi zao na ada zao na kuangalia yapi anayohitaji Allah Mola wao Muumba wao na kupwekesha nyoyo zao kwa ajili ya Allah Mukufu.
  3. kutarajia kwa wenye nyoyo kutumai kukutana na Allah kwa kufungana nyoyo zao na kumtamani Allah pekee na kutaraji huku ndiko kwa hali ya juu zaidi amesema Allah Mtukufu: {Anayependa kukutana na mola wake naafanye vitendo vizuri wala asimshirikishe yoyote katika ibada ya mola wake.} [A-lkahf : 110]

Asema Allah Mtukufu: {Mwenye kutaka kukutana na mwenyezi mungu , basi hakika ajali ya Mwenyezi Mungu itafika tu naye ni mwenye kusikia na mwenye kujua.} [Al-ankabuut :5]

Mwenye kutaraji kitu hukitafuta

Kushikamana kwa kumtambua Allah na majina yake na sifa zake

Mwanadamu mwenye kutaraji hua ameshikana na kumtii Allah, mwenye kutekeleza kulingana na maekezo ya imani yake, akitarajia kutoka kwa Allah Mtukufu asije akamwangamiza na akitarajia kukubaliwa matendo yake wala yasije yakarudishwa yasikubaliwe, na kuongezewa malipo na ujira wake ,kwahio ni mwenye kujitahidi kwa kufanya sababu ambazo zitamuhakikishia haya kulingana na uwezo wake, anatarajia rehema za Mola wake; kwasababu anautambuzi wakutosha wa kumjua Mola wake na sifa zake na majina yake,anajua kuwa yeye ana amiliana na Mola Mwenye rehema na mapenzi mwenye shukrani na mkarimu mwenye kutoa mwenye kusamehe anayejua kila kitu, huyu anateseka hapa duniani lakini anatarajia amani ya Allah siku wakikutana.

Matunda ya kutarajia 

  1. inakuza kwa mwenye kutarajia kujitahidi katika kutekeleza zitendo vizuri na kumtii Allah.
  2. inamfundisha mtu kushikamana na twaa ya Allah; hata kama hali zitageuka au kutokee dhiki.
  3. inamfundisha mtu kuendelea kuelekea Allah kwa kumuomba na kumnyenyekea katika kumuomba na kukariri kumuomba.
  4. inadhihirisha utumwa na umasikini na haja ya mja kwa Allah Mwenye nguvu na utukufu, kwamba mwanadamu hawezi kususia fadhila na wema wake Allah hata kwa mda kidogo.
  5. kutambua na kuwa na yakini kwa kuwepo kwa Allah ,na ukarimu wake. kwasababu yeye Allah ni mkarimu zaidi kwa mwenye kumuomba anatoa bila mipaka, naye anapenda kwa waja wake wamuombe na wamtarajie na wamlilie.
  6. Kutarajia kunamueka mja kwenye mapenzi ya Allah na kumfikisha katika ukamilifu wa mapenzi hayo, kila anapozidi kumtaraji Allah na kupata anachokitarajia, huongezeka mapenzi yake kwa Mola wake na kumshukuru na kuridhia, na haya ndio matakwa ya imani na nguzo za ibada kwa mja.

Kila wakati mwenye kumtarajia Allah anakuwa anaraghba matumaini na kuogopa anatarajia fadhila za Allah, akiwa na dhana nzuri kwa Allah aliye juu na Mwenye nguvu .

Muumini alimdhania Mola wake mazuri ndio akafanya vitendo vizuri na mtu muovu alikuwa na dhana mbaya kwa mola wake ndio maana akafanya vitendo vibaya.

Miongoni mwa dhana nzuri kwa Allah ni kutambua kuwa Allah hampotezi atakaye muelea yeye.

  1. Ni msukumo kwa mja kufikiya daraja ya kushukuru ,kwasababu kunamsukuma afikiye daraja ya kushukuru neema za Allah; ambayo ndio daraja ya hali ya juu ya uchaji Mungu.
  2. kuyatambua majina ya Allah na sifa zake , kwani yeye ni Mwenye rehema Mkarimu Mwenye kuitikia Mzuri Mpwasi[Tajiri] ametakasika Allah na sifa zote za upungufu, ni Mola mkubwa alioje Mola wetu huyu!
  3. Ni sababu ya kuyapata mja anayoyatarajia,na kufikia matwaka inasaidia kuongeza msukumo na kuomba kuongezewa na kuelekea Allah , hivi mja hataacha kuwa katika kuongezewa imani na kuwa karibu na Allah.
  4. Kufurahi waumini siku ya kiyama kwakufikia wanayoyatarajia kwakupata radhi za Allah na pepo na kumuona Allah Mtukufu yote haya yatakuwa kulingana na matarajio ya waja na khofu zao kwa Allah hapa duniani

Hukumu zake na tanbihi zake 

  1. Kumuogopa Allah kunaenda sambamba na kumtarajia kama vile kutarajia kunaambatana na khofu ya Allah, hivi ndio inapatikana kutaraji sehemu ambayo ilikuwa ni khofu na kinyume chake pia. {Mumekuwaje hamuweki heshimaa ya Mwenyezi Mungu} [Nuh : 13]

Akasema Allah Mtukufu: {Waambie walio amini wawasamehe wale wasio zitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyo kuwa wakiyachuma.} [Al-jathiyah :14]

Hawaogopi matukio ya Allah kama yalivyo watokea watu waliokuwa kabla yao miongoni mwa kuangamiza na kuvunja vunja.

  1. kutarajia ni dawa ambayo tunaihitaji wakati :

-Kama mtu amekata tamaa mpaka akaamua kuacha ibada.

-kama utamghilibu uoga mpaka akadhurika nafsi yake na watu wake, paka khofu yake inapita kiwango cha kisheria, hapa ndipo lazima apate kitu kitakacho mueka sawa nacho ni kutarajia kwa Allah hali ambayo ni yakawaida kwa waumini.

  1. kutarajia ni kinyume cha kukata tamaa, na kukata tamaa ni kukataa rehema za Allah na kuacha kutafuta rehema za Allah, na hiki ni chanzo cha upotevu, na ukafiri, asema Allah alietukuka: {Wala msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hawakati tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri.} [Yusuf 87]

Kama italetwa mizani na kupima khofu ya muumin na kutaraji kwake zitakuwa sawa sawa

Siridhii kuona hisabu zangu nafanyiwa na babangu, Mola wangu ni bora kwangu kuliko babangu.

Imamu Sufiyan Athauri.

Haitimii ibada yoyote isipokuwa kupatikane khofu na kutarajia, kwa ajili ya khofu anakatazika mtu na makatazo ya Allah, na kwa ajili ya kutarajia anaongeza kumtii Allah.

Imamu Ibn Kathir

Marejeo 

  1. Je kutarajia rehema za Allah kunapelekea kwenye aamali? Eleza hayo kulingana na upeo wa aya yake Allah:{ Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.} [A-lkahf : 110]
  2. Je kumtarajia Allah kuna maanisha kutomkhofu Allah? Ama khofu ndio haiambatani na kutarajia?
  3. Taja majina na sifa za Allah unazozijua ambazo zinalazimisha kumtarajia Allah