Kumpwekesha Allah kunadhihirika katika mwenendo wa mwanadamu na vitendo vyake. Kama ilivyo moyoni mwake, na ya kumcha Allah inadhihirika katika mwenendo wake pekee au yeye na wenzake, kwa hiyo uhai wote ni athari za imani na tawhiid na ibada. Amesema Allah Mtukufu:
{Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu} [Adh-dhariyat : 56]
Na miongoni mwa athari zake zilizo wazi katika mwenendo wa mwanadamu hasa:
Ya kwanza: athari khasa kwa mtu pekee:
Tawhiid [kumpwekesha Allah] ndilo jambo la pekee kubwa linaloleta tahara [usafi] kwa muumini, ndiomana Allah anaipenda, amesema Allah Mwenye Nguvu na Utukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa} [Baqarah :222]
Amesema Mtume [s.a.w] «Usafi ni nusu ya imani»(Imepokewa na muslim)
Tohara [usafi] ni nusu ya imani, kwasababu ni aina moja muhimu ya imani, na Allah anapenda aina zote za tohara [usafi]basi iwe ni:
Ambayo inakusudiwa kuitahirisha nafsi kutokana na athari za madhambi na maasi na kumshirikisha Allah, nayo ni kwa kutubia toba ya kikweli kweli , na kutahirisha moyo kutokana na uchafu wa shirki, na shaka, na hasadi, na chuki, na ugonvi, na kiburi, na mtu kujitahirisha kutokamana na vitu hivi haiwezikani mpaka ipatikane ikhlasi [kufanya vyote hivi kwa ajili ya Allah pekee], na kupenda kheri na upole na unyenyekevu na ukweli, na kufanya kwa kutaraji radhi za Allah kupitia vitendo hivi.
Unakusudiwa usafi huu kuondoa uchafu na hadadhi.
Kuondoa najisi na uchafu:
Inakuwa kwakuondoa najisi kwa kutumia maji masafi, nguoni au mwilini au sehemu utakayotekeleza ibada, na kila kinacho ingia chini ya hivi.
Kuondoa hadathi
Inakusudiwa hapa kutia udhu, na kuoga na kutayamam; kwa ajili ya kusali, au kusoma quran, au kutufu alqa’aba nyumba yake Allah, au kumtaja na kumkumbuka yeye Allah Mtukufu, ama aina nyebgine za ibada.
Amesema Mtume [s.a.w] ‘usafi ni nusu ya imani’ [imepokewa na Muslim]
Kumpwekesha Allah kunadhihirika wazi katika sala ambayo ndio mawasiliano pekee baina ya mja na Mola wake, hapo ndipo mja anamuonyesha Mola wake jinsi gani anamtii na kumpenda na kunyenyekea kwake, kwahio sala ni nguzo kubwa katika nguzo za uisilamu baada ya shahada mbili, nayo ni nguzo ya dini na nuru ya yakini, ndani ya sala nafsi inatengezeka na kifua kukunjuka na moyo kutulia, sala ni kizuizi cha kufanya maovu na ni sababu ya kufutiwa makosa, nayo ni vitendo maalumu kwa wakati maalumu vinavyo funguliwa kwa takbir na kumalizwa kwa salamu.
Na mwenye kuacha sala kwa kuikanusha amempinga Allah na Mtume wake, na kukataa amri za quran, na haya yanaenda kinyume na asili ya imani, ama Yule anaye kubali kuwa ni lazima kusali lakini akaiacha kwa uvivu tu basi ameihatarisha nafsi yake kwa hatari kubwa na makemeo makali, amesema Mtume [s.a.w] «Tofauti ilioko baina ya muislamu na ushirikina na ukafiri ni kuacha sala»(Imepokewa na Muslimu)
Wamesema baadhi ya wanavyuoni kuwa ni ukafiri pia, lakini si ukafiri ule mkubwa unaomtoa mtu katika uislamu, lakini hata hivyo ni dhambi kubwa na ni moja wapo ya yale madhambi yenye kuangamiza.
Swala iko na athari kubwa sana miongoni mwazo:
Amesema Mtume[s.a.w] ‘Swala ni nuru’ [imepokewa na Albaihaqi]
Ni amali bora ambayo mja anajikaribisha kwa Allah.
Akasema tena Mtume [s.a.w]« sala ni nuru» (Imepokewa na Albaihaqi)
Zaka ni kutahirisha na kukuza nafsi na mali na jamii,
Mtukufu: {Simamisha sala kwa kunitaja.} [Taha :14]
Katika kukuza na kutahirisha, usafi wa nafsi ya mja anayempwekesha Mola wake unamfanya atoe mali yake na kuisafisha kupitia zaka, kwani zaka ni haki ya lazima kutoka kwa matajiri kupatiwa mafakiri, na wanaofanana nao, kwalengo la kumridhisha Allah na kuitakasa nafsi na kutendea wema walio na haja.
Zaka iko na umuhimu sana katika uislamu, ndio maana likawa lengo la kuekwa zaka laonyesha umuhimu wake. Na atakae chunguza katika sababu za zaka ataona umuhimu wa nguzo hii tukufu na athari zake kubwa, miongoni mwa hizo athari:
Yamekuja mambo haya kwenye maandishi, yanayoonyesha wazi ulazima wa kutoa zaka, na akaeka wazi Mtume [s.a.w] kuwa zaka ni miongoni mwa nguzo na misingi ya uislamu muhimu sana ambayo uislamu ulijengwa kwazo, ndio maana ikafanywa kuwa nguzo ya tatu katika nguzo za uislamu. Amesema Allah Mtukufu: {Na simamisheni sala [enyi mayahudi] na toeni zaka na inameni pamoja na wanaoinama [yaani kuweni waislam]} [Albaqarah :43]
Na akasema tena, Allah Mtukufu: {Na simamisheni sala na toeni zaka; na kheri mtakazozitanguliza, kwa ajili ya nafsi zenu, mtazikuta kwa mwenyezi mungu. Hakika mwenyezi mungu anayaona [yote]mnayoyafanya.}
[Al baqara : 110]
Na katika hadiith ya Jibril mashuhuri: «Uislamu ni kushuhudia kuwa hakuna wakuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wake, na kusimamisha sala na kutoa zaka na kufunga mwezi wa ramadhani na kuhiji nyumba kongwe [maka] kwa mwenye uwezo.» (Imepokewa na Muslim)
Amesema Mtume [s.a.w] «Umejengwa uislamu kwa mambo manne : kushudia ya kuwa hakuna wakuabudiwa ila Allah na Muhamad ni Mtume wa Allah na kusimamisha sala na kutoa zaka na kuhiji na kufunga mwezi wa ramadhani» (Imepokewa na Albukhari)
Maandishi haya na mfano wake yanaonyesha wazi kabisa kuwa zaka ni moja katika nguzo za kiislamu, na misingi yake mikubwa, ambayo haukamiliki uislamu isipokuwa hiyo.
Allah alifaradhisha funga na kuifanya kuwa moja ya nguzo za kiislamu, nayo ni kujizuiya na vivunja saumu kwa nia ya ibada kutokea kwa asubuhi hadi kuzama kwa jua. Amesema Allah Mtukufu: { Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku.} [Albaqarah : 186]
Na kukitisha imani katika moyo wa mja na kumpwekesha Mola wake ni sababu ya kutekeleza aliyofaradhishiwa, kwa kufuata neno lake Allah Mtukufu: { Enyi mlioamini mumelazimishwa kufunga [saumu] kama walivyolazimiswa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu} [Al baqarah 183]
Wanafurahia wenye kumpwekesha Allah kwa kufunga na kupatilizia katika hilo, amesema Allah katika hadiith qudsi: «kila aamali ya mja wangu ni yake isipokuwa saumu hiyo ni yangu na mimi ndiye nitailipa.» (Imepokewa na Albukhari)
Saumu ni chuo chakujenga imani katika nafsi .
Athari za saumu kwa mja ni nyingi sana miongoni mwazo:
Kumpwekesha Allah kunadhihirika katika Hajj, Hajj nimiongoni mwa ibada ambazo zinamuongezea muilsamu tawhiid yake, na kujipamba na imani kamili; katika hajj mtu anatangaza tawhiid yake aingiapo hajj tu akisema: ”nimeitikia mwito ewe Mola wangu nimeitikia huna mshirika Mola wangu nimeitikia”. Si mwanzo wakuingia tu peke yake, bali katika kila sehemu na kila hatua anakariri maneno haya, ili arudi wakati wa kurudi akiwa amefutiwa madhambi yake yote, na kurudi kama siku aliyozaliwa na mamake, kwasababu ya tawhiid tu na kuitangaza, hajj ni kukusudia kwenda nyumba tukufu, katika masiku maalumu ya hajj, kwa nia ya kutekeleza ibada ya hajj, kama ilivyofudhishwa kutoka kwa Allah, na kama alivyo hiji Mtume [s.a.w] nayo ni faradhi kutoka kwake Allah kwa viumbe vyake, iliyothibiti kwa maandiko ya qurani na suna zake Mtume [s.a.w] na maafikiano ya waislamu wote.
Miongoni mwa athari za hajj kwa maisha ya mwanadamu:
Amesema Mtume [s.a.w] hakika imeekwa tawafu [kuzunguka alka’aba] na kuenda swafa na marwa , na kurusha vijiwe katika jamarat, kwa ajili ya kuendeleza kutaja jina lake Allah [imepokewa na Ahmed]