1-Kuokolewa Kutoka Shaka Na Utesi, Atapatikana Vipi Na Shaka Mwenye Kujua Kuwa Yuko Na Mola Wa Kila Kitu, Naye Ndiye Aliye Muumba Kisha Akamtengeza Vizuri Na Akamfadhilisha Na Kumtukuza, Na Akamfanya Khalifa Hapa Ardhini, Na Akamdhalilishia Kila Kitu Mbinguni Na Ardhini, Na Akampatia Neema Zake Zilizo Dhahiri Na Zilizo Jificha, Ndipo Mwanadamu Akatumaini Kwa Mola Wake Na Akapata Ujirani Wake, Na Akajua Kuwa Maisha Ya Dunia Ni Mafupi Yamechanganyika Kheri Na Shari Uadilifu Na Udhalimu Tamu Na Chungu.
Ama Waliopinga Tawhiid Arrububiya, Walio Na Shaka Kwa Kukutana Na Allah, Maisha Yao Hayana Ladha Yoyote Wala Maana, Ni Wasi Wasi Tu, Na Maswali Mengi Bila Majibu, Kwasababu Hawana Nguzo Wanayo Itegemea, Basi Akili Zao Ziko Katika Hali Ya Wasi Wasi Daima Hata Kama Mtu Ni Mjanja Kiwango Gani Lakini Wasiwasi Haumuachi Hii Ndio Adhabu Ya Kidunia Na Moto Wa Dunia Unaochoma Nyoyo Zao Usiku Kucha.
Imani Inakaribisha Mafanikio2-Utulivu WA Moyo: Hakika Utulivu Uko Na Msingi Mmoja Tu Nao Ni Kumuamini Allah Na Siku Ya Mwisho, Imani Ya Kweli Kweli Iliyo Ndani Ya Moyo Ambayo Haipatikani Na Shaka Wala Haiharabiwi Na Unafiki. Hii Ndiyo Inayoonekana Sasa, Na Kutiliwa Nguvu Na Yaliyo Jaa Katika Historia, Na Anayoyahisi Na Kuyaona Kila Mtu Muadilifu Katika Nafsi Yake Na Wenzake, Hakika Tumejuwa Kuwa Wengi Wanao Kuwa Na Wasiwasi Na Dhiki Ya Maisha Na Matatizo Na Kuhisi Kupotea Na Kukosa Raha, Wengi Wao Ni Watu Walio Nyimwa Neema Ya Kumuamini Allah Na Kutoyakinisha Ahadi Zake, Hakika Maisha Yao Hayana Ladha Yoyote Wala Utamu Wowote , Hata Kama Mtu Atazungukwa Na Starehe Za Aina Tofauti Tofauti, Kwa Sababu Wao Hawatambui Maana Ya Maisha Yao, Wala Hawajui Siri Yake, Sasa Vipi Wata Furahia Na Kusherehekea Utulivu Wa Moyo Na Ukunjufu Wa Kifua?!. Hakika Utulivu Huu Ni Matunda Miongoni Mwa Matunda Ya Imani. Na Tawhiid Ni Mti Mzuri Unao Toa Matunda Yake Kila Wakati Kwa Idhini Yake Allah, Kwahiyo Hizi Ni Baraka Za Mbinguni. Allah Anaziteremsha Kwa Nyoyo Za Waumini, Ili Wawe Imara Wakati Watu Wengine Wakitatizika Na Kutingishika, Wakakubali Na Kuridhia Kwa Kigawanyo Cha Allah Wengine Watakapochukia, Na Wawe Na Yakini Na Ahadi Zake Allah Wakati Wengine Wakiwa Na Shaka, Na Wawe Na Subira Watu Watakapo Shindwa Na Kusubiri, Na Wawe Wenye Akili Timamu Wakati Wengine Wakichanganyikiwa, Huu Ndio Utulivu Ndio Ulioimarisha Moyo Wa Mtume (S.A.W) Siku Ya Kuhama Makka Kwenda Madina. Haukumsibu Uoga Wala Wasiwasi Wala Humumu Zozote Wala Huzuni Wala Hakuwa Na Shaka Dhidi Ya Ahadi Zake Allah, Asema Allah Mtukufu: { Kama Hamtamnusuru (Mtume), Basi Mwenyezi Mungu Alimnusuru Walipomtoa Wale Waliokufuru; Alipokuwa(Mmoja Tu Na Mwenziwe) Wa Pili Wake, (Peke Yao); Walipokuwa Wote Wawili Katika Pango; (Mtume) Alipomwambia Sahibu Yake“ Usihuzunike} (At-Tawba :40)
Mwenye Kutosheka Na Allah Watu Wengine Watamuhitajia.Hakika Alipatwa Abubakar Na Hisia Za Uoga Na Huruma Lakini Si Kwa Nafsi Yake Na Uhai Wake Bali Uhai Wa Mtume (S.A.W) Na Da’awa Ya Kiislamu Na Tawhiid, Mpaka Ikafikia Kusema Abubakar: “Na Maadui Wamelizunguka Pango.” : “Ewe Mtume Wa Allah Kama Angaliangalia Mmoja Wao Chini Ya Miguu Yake Tu Basi Angalituona,”Akasema Mtume (S.A.W) Ewe Abubakar Wadhania Nini Wawili Ambaye Watatu Wao Ni Allah.” (Imepokewa Na Muslim)
Na Utulivu Huu Ni Roho Inayotoka Kwa Allah Na Nuru Yake Inayo Mtuliza Muoga, Na Kumtumainisha Mwenye Wasiwasina, Kumliwaza Aliye Na Huzuni,Na Kumpumbazisha Aliyechoka, Na Kumpa Nguvu Mnyonge, Na Kumuongoa Aliye Changanyikiwa, Utulivu Huu Unaelekeza Peponi Ili Allah Awafungulie Waumini Katika Waja Wake, Humo Peponi Watapulizwa Na Ubaridi Nyororo Na Kuangaziwa Na Nuru Yake Na Kupulizwa Na Manukato Yake, Ili Allah Awaonjeshe Katika Malipo Ya Yale Waliyoyafanya Katika Mambo Ya Kheri, Na Awaonyeshe Mfano Mdogo Wa Yale Mengi Yanayo Wasubiri Katika Neema , Kwahiyo Wataneemeka Kutokana Na Baraka Hizi Kwa Amani Na Utulivu Na Riwaza Maalumu .
Kila Unapokuwa Uhusiano Wako Na Allah Ni Dhaifu Itakuwa Ni Sababu Yaugomvi Na Kutoelewana.3-Uhakika Wa Allah: Kila Kitu Kiko Mikononi Mwake Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu, Miongoni Mwavyo Manufaa Na Madhara Basi Allah Ndiye Muumba Wa Kila Kitu, Naye Ndiye Mwenye Kuruzuku Mwenye Kumiliki Na Kuendesha Mambo Ya Viumbe Vyake,Yuko Nazo Funguo Za Mbingu Na Ardhi, Kwahiyo Atakapo Jua Muumin Kwamba Halimsibu Ila Alilomuandikia Allah La Kheri Au La Shari, Manufaa Ama Madhara, Na Kwamba Kukusanyika Kwa Viumbe Wote Kwenda Kinyume Na Alivyo Kadiria Allah Hakuna Faida Yoyote, Ndio Twafahamu Kuwa Allah Pekee Ndiye Mwenye Kuleta Manufaa Na Kuleta Madhara, Mtoaji Na Mwenye Kuzuia, Mambo Ambayo Yanaongeza Uaminifu Kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu Na Utukufu Na Kuitukuza Tawheed Yake, Kwahio Ndio Maana Allah Akakemea Na Kukataza Mwenyekuabudu Asiyenufaisha Wala Kudhuru Wala Hatoshelezi Mahitajio Ya Wanao Muomba Kwa Kitu Chochote : Ametakasika Allah Aliyesema: { Funguo Za Mbingu Na Ardhi Ziko Kwake, Na Wale Waliozikanusha Aya Za Mwenyezi Mungu Hao Ndio Wenye Hasara. } (Az-Zumar: 63)
4-Kumtukuza Allah: Athari Hii Iko Wazi Katika Maisha Ya Mwenye Kumuamini Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu, Mwenye Kumpwekesha Kwa Ibada Na Lengo Na Maombi Na Matakwa Yake Yote. Na Anapo Zingatia Muumini Yaliyoko Kwa Allah Miongoni Mwa Ufalme WA Mbinguni Na Ardhini Hana Lakusema ILA Kusema Tu: {Mola Wangu Anakijua Vyema Kila Kitu} (Al An-Am: 80), Na Anasema: {Mola Wetu Hakuviumba Hivi Bure Utukufu Ni Wako} (Aali Imran: 191)
Katika Moyo Kuna Upungufu Hakuna Wakuujaliza ILA Mtu Kuelekea Kwa Allah, Na Kuna Upweke Hakuna Wakuondoa Ila Riwaza Yake Allah Katika Sehemu Pweke, Na Kuna Huzuni Hakuna Wakuondoa Ila Furaha Ya Kumtambua Yeye Na Kuamiliana Naye Kwa Ukweli.Yote Haya Yaonyesha Jinsi Gani Nyoyo Za Hawa Waja Zilivyo Shikamana Na Allah Mola Wao Na Muumba Wa Kila Kitu Mwenye Nguvu Na Utukufu, Na Vipi Hawa Waja Wanavyo Jitolea Muhanga Ili Kumridhisha Allah Na Kutukuza Sharia Zake Na Maamrisho Yake, Bila Kutia Shaka Kwa Wale Wasiomiliki Chochote Si Mbinguni Wala Ardhini Si Katika Manufaa Yao Wala Yawenziwao Hata Japo Punje Moja, Yote Haya Ni Kumuadhimu Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu, Na Ni Athari Za Tawhiid Arrububiya (Ya Ulezi) Kwa Waumini.