Ulimwengu Wote Wakiri Na Kukubali Na Kuamini Bali Hata Kusema Kuwepo Kwa Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu. Asema Allah Mtukufu: {Mitume Wao Wakasema;”Je! Mnamfanyia Shaka Mwenyezi Mungu. Muumba WA Mbingu Na Ardhi? Yeye Anakuiteni Akusameheni Dhambi Zenu Na Akupeni Muhula Paka Muda Uliowekwa.”Wakasema:”Hamkuwa Nyinyi ILA Ni Watu Kama Sisi.Mnataka Tu Kutuzuilia Na Yale Waliokuwa Wakiyaabudu Baba Zetu. Basi Tuleteeni Hoja Zilizo Wazi} (Ibrahim: 10)
Muumini WA Kweli Ni: Yule Aliyeyakinisha Kuwa Allah Mungu Aliye Na Uwezo, Na Akayakinisha Kuwa Yeye Tu Ndiye Yuwafaa Kuabudiwa.Vipi Wanataka Hoja Naye Allah Ni Hoja Tosha Kwani Yeye Ni Hoja Kwa Kila Kitu Kwa Nguvu Zake Na Uwezo Wake.
Huwezi Kumsifu Allah Isipokuwa Kwa Fadhila Zake Na Neema Zake, Nawe Kwa Hali Zote Una Muhitaji Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu.Hata Kama Tukiacha Haya Na Kuleta Hoja Za Kuthibitisha Kuwepo Kwake Allah; Tunapata Hoja Nyingi Tu Miongoni Mwazo:
Viumbe Waliumba Kwa Kawaida Wamuamini Allah Aliye Waumba, Ukawaida Huu Hauondoki ILA Kwa Mtu Aliyemfuta Na Kumuondoa Allah Kutoka Kifuani Kwake Na Akilini Mwake. Na Miongoni Mwa Dalili Kuu Zinazo Tuonesha Hivyo Kwamba Kawaida Na Maumbile Yana Kubaliana Na Kuwepo Kwake Allah Ni Maneno Yake Mtume (S.A.W) &" Kila Mtu Anazaliwa Na Maumbile Ya Dini Ya Kiislamu Lakini Wazazi Wake Ndio Humbadilishia Dini Wakamfanya Akawa Myahudi Au Mkristo Au Mwenye Kuabudu Moto, Kama Vile Mnyama Anavyo Zaliwa Masikio Yake Huwa Yako Sawa. Je! Mliwahikuona Mnyama Kazaliwa Masikio Yamekatwa? &"(Imepokewa Na Bukhari)
Na Kila Kiumbe Kinakiri Tawhiid (Kumpwekesha Allah) Kwa Maumbile Yake. Asema Allah Mtukufu: {Basi Uelekeze USO Wako Katika Dini Iliyo Sawasawa – Ndilo Umbile Mwenyezi Mungu Alilowaumbia Watu, Hakuna Mabadiliko Katika Maumbile Ya Viumbe Vya Mwenyezi Mungu. Hivyo Ndivyo Dini Ilivyo Haki, Lakini Watu Wengi Hawajui} (Ar Rum: 30), Hizi Ni Hoja Na Dalili Za Kimaumbile Zinazoonyesha Kuwepo Kwa Allah Mtukufu.
Na Hoja Za Kimaumbile Zinazoonyesha Kuwepo Kwa Allah Zina Uzito Zaidi Kuliko Dalili Zengine Zote, Kwayule Ambaye Hajabebwa Na Shetani, Ndio Akasema Allah Mtukufu: {Ndilo Umbile Mwenyezi Mungu Alilowaumbia Watu} (Ar Rum: 30)
Baada Aliposema: {Basi Uelekeze USO Wako Katika Dini Iliyo Sawasawa}(Ar Rum: 30)
Kwahiyo Umbile Lililo Salimika Linashuhudia Kuwepo Kwa Allah, Ama Aliye Tekwa Na Mashetani Yaweza Kumzuia Dalili Hii Na Akahisi Kuwa Anahitaji Dalili Hii,Lakini Akipatikana Na Shida Au Majanga Mazito Uelekeza Mikono Yake Na Macho Yake Mbinguni Akiomba Aokolewe Na Asaidiwe Na Mola Wake Moja Kwa Moja Kwa Umbile Lake Na Umbo Lake Lililo Kamilika.
Miongoni Mwa Hoja Nzito Za Kuwepo Kwa Allah Muumba, Ni Dalili Za Kiakili Ambazo Hakuna Mwenye Kuzikataa ILA Mwenye Inadi (Kupinga) Tu, Miongoni Mwazo:
1-Kila Kiumbe Kinaye Muumba, Kwasababu Viumbe Vyote Lazima Viwe Na Muumba Aliye Viumba;Kwasababu Haviwezi Kujiumba, Na Kujileta Vyenyewe, Wala Haviwezi Kupatikana Kwa Sudfa (Ghafla), Kwahiyo Haviwezi Kujiumba Vyenyewe, Kwasababu Kiumbe Hakiwezi Kujiumba Chenyewe, Kwasababu Kabla Hakijaumbwa Huwa Hakipo Vipi Kitakuwa Ndicho Kilijiumba?!; Kwasababu Kila Kilichopo Lazima Kililetwa, Na Kupatikana Kwake Katika Hali Hii Madhubuti Tena Imara Kabisa Na Kushikana Kwasababu Na Mwenye Kusababisha Na Kushikana Kwa Baadhi Ya Viumbe Na Baadhi Yao Yote, Haya Yakataa Kuwa Ulimwengu Huu Ulipatikana Kwa Sudfa Tu, Kila Kiumbe Lazima Kiwe Na Muumba, Kama Haviwezi Kujileta Vyenyewe Viumbe Hivi Wala Kupatikana Kwa Sudfa, Inalazimu Kuwa Vinamuumba Ambaye Ni Allah Mola Wa Viumbe Vyote, Na Alitaja Dalili Hii Ya Kiakili Allah Aliposema: { Je! Waliumbwa Pasipo Kitu, Au Wao Ndio Waliojiumba. } (At-Tur: 35)
Yaani: Kwani Wao Hawajaumbwa Na Muumba Ama Walijiumba Wenyewe, Jawabu Aliyewaumba Ni Allah Mtukufu, Kwahiyo Aliposikia Jubeir Ibn Mat’am Mtume (S.A.W) Akisoma Sura “T-Tuur” Alipofika Katika Aya Hii: { Je! Waliumbwa Pasipo Kitu, Au Wao Ndio Waliojiumba. Au Wameumba Mbingu Na Ardhi? Bali Hawana Yakini (Ya Jambo Lolote)} (At-Tur: 35-37), Na Jubeir Wakati Huo Alikuwa Bado Ni Mshirikina Akasema: “Kidogo Moyo Wangu Uruke” (Imepokewa Na Bukhari)
2-Aya Zake Allah Zilizo Dhahiri Katika Ulimwengu Na Viumbe Vyake, Amesema Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu: {Sema Angalieni Kumetokea Nini Mbinguni Na Ardhini} (Yunus: 101)
Kwasababu Kuangalia Mbinguni Na Ardhini Ndio Kunaweka Wazi Kuwa Allah Ndiye Muumba, Na Inatilia Mkazo Wa Uungu Wake Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu, Aliambiwa Mbedui Mmoja Kutoka Mashambani: Kwa Kitu Gani Ulimjua Mola Wako? Akasema: Athari Za Nyayo Zinaonesha Kupita Kwa Mtu, Na Choo Cha Ngamia Kinaonesha Kupita Kwa Ngamia, Je! Mbingu Ilyojaa Nyota, Na Ardhi Iliyo Na Njia Nyingi, Na Bahari Zilizo Na Mawimbi Mbona Zisioneshe Kuwepo Mwenye Kusikia Na Kuona?
Mwanadamu Anashangaa Na Kuduwaa Atakapo Angalia Maajabu Ya Vitu Vya Ghaibu Visivyoonekana, Ata Kama Elimu Yake Itafika Wapi Katika Elimu Yakidunia, Ispokuwa Imani Pekee Ndio Inaweza Kutambua Uwezo Huu.3-Nidhamu Ya Ulimwengu Na Uimara Wake, Hii Ni Dalili Tosha Kuonyesha Aliyeiumba Ni Mola Mmoja, Na Mfalme Mmoja, Na Mungu Mmoja. Viumbe Hawana Muumba Ila Yeye Tu, Na Hawana Mungu Ila Yeye, Kama Vile Nimuhali Kupata Miungu Miwili Na Waumba Wawili, Kwahiyo Kutambua Kuwa Kupatikana Ulimwengu Na Miungu Wawili Wenye Kufanana Inakuwa Ni Muhali Yenyewe. Na Mambo Haya Yamekita Katika Maumbile, Yenye Kujulikana Kwa Akili Umuhali Wake Hivyo Hivyo Kuwepo Na Mola Wa Pili Ni Kitu Kisicho Wezikana.
Sharia Zote Zinaonyesha Kuwepo Kwa Allah Muumba Ambaye Elimu Yake Imekamilika Na Hikma Zake Zimekamilika, Na Rehema Zake Pia, Kwasababu Sharia Hizi Lazima Awepo Mwenye Kuzieka, Na Mwenye Kuzieka Ni Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu . Anasema Allah Mtukufu: {Enyi Watu! Mwabuduni Mola Wenu Ambaye Amekuumbeni Nyinyi Na Wale WA Kabla Yenu, Ili Mpate Kuokoka. Mwenyezi Mungu Ambaye Amekufanyieni Hii Ardhi Kuwa Kama Bustani Na Mbingu Kuwa Kama Paa, Na Akateremsha Maji Kutoka Mawinguni; Na Kwa Hayo Akatoa Matunda Yawe Riziki Zenu. Basi Msimfanyizie Mwenyezi Mungu Washirika, Na Hali Nyinyi Mnajua.} (Al-Baqarah 21-22), Na Viabu Vya Mbinguni Vyote Vimeeleza Kuhusu Mambo Haya.
Miongoni Mwa Dalili Za Wazi Kabisa Za Kujua Kuwepo Kwa Allah Ni Dalili Za Kihisia Zilizo Wazi Zinazo Onekana Kwa Kilamwenye Macho Na Akili Miongoni Mwazo:
1-Kukubaliwa Kwa Dua: Mwanadamu Anamuomba Allah Akisema: Ewe Mola Wangu Ndio Aombe Akitakacho, Kisha Allah Anamtakabali, Na Dalili Hizi Za Kihisia Zinaonyesha Kuwepo Kwa Allah, Mwenyewe Mwanadamu Hakuomba Alipoomba Ila Allah, Naye Allah Akamtakabalia Na Akashuhudia Mwenyewe Kwa Jicho Lake,Nasi Twasikia Tangu Zamani Na Hata Sasa Mifano Mingi Ya Watu Walio Takabaliwa Na Allah Maombi Yao, Na Jambo Hili Liko Na Latokea , Hili Laonesha Kuwa Allah Yuko Na Ni Dalili Ya Hisia Na Katika Qurani Kuna Mifano Mingi Kama Hii : Miongoni Mwazo: { Na (Mtaje) Ayyubu, Alipomwita Mola Wake (Akasema)” Mimi Imenipata Dhara, Nawe Ndiwe Unaye Rehemu Kuliko Wote Wanaorehemu. Basi Tukamkubalia (Wito Wake)} (Al-Anbiyaa: 83-84), Na Aya Nyingine Nyingi.
Kukataa Kuabudu Allah Ni Ugonjwa WA Akili Na Tatizo Katika Fikra Za Mtu.2-Kuwaongoza Viumbe Katika Mambo Yaliyo Na Siri Ya Maisha Yao, Nani Aliye Muongoza Mwanadamu Alipozaliwa Kujua Wapi Pa Kunyonya? Na Ninani Aliyemuongoza Hud’hud Mpaka Akaona Sehemu Ya Maji Chini Ya Ardhi Jambo Ambalo Hakuna Mwengine Mwenye Kuona?
Kukataa Kuabudu Allah Ni Ungonjwa WA Akili Na Tatizo Katika Fikra Za Mtu Na Kupotea Katika Maisha.Hakika Yeye Ni Allah Aliyesema: {Musa Akasema: Mola Wetu Ni Yule Aliyekipa Kila Kitu Umbo Lake Kisha Akakiongoza (Kufuata Kinachowafiki Umbo Lake Hilo)} (Taha: 50)
Alama Walizokuja Nazo Manabii Na Mitume Nayo Ni Miujiza Aliyotilia Nguvu Ujumbe Wake Na Wajumbe Wake, Na Akawachagua Kwa Hilo Kuliko Watu Wengine, Kila Nabii Alimtuma Allah Akiwa Na Muujiza Unaotilia Nguvu Utume Wake Kuonesha Ujumbe Aliokuja Nao Watoka Kwa Allah Muumba Mmoja Asiye Na Shaka Wala Hakuna Mwengine Asie Kuwa Yeye (Alifanya Haya).